
Akizungumza na www. eatv.tv Mtulia amesema wanashukuru kwa kuondoka kwa Mbuge huyo kwa sababu mpaka mtu anapoamua kwenda sehemu nyingine anakuwa amefanya maamuzi kwa muda mrefu na siku ya kuondoka ndiyo yanakuwa matokeo ya kile alichokitamani muda mtefu.
Mtolea amesema kuwa ni hatari zaidi kwa kipindi alichokuwepo ndani ya chama chao huku akiendele kufanya kazi ya maadui katikati yao.
Mbunge huyo amesema kuwa "Siwezi kusema kuwa hakuna pengo aliloliacha kwani kila mtu ana mabaya na mazuri yake. Kwanza kaniacha mpweke kwenye jiji awali tulikuwa wabunge wawili sasa hivi nimebaki Mbunge wa CUF mmoja hilo kwangu ni pigo, lakini mtu akiamua kuhama chama ni bora zaidi kwani mtu anapoamua kuhama chama inamaana alikuwa anakitamani muda mrefu hivyo ni vyema adui ukamjua mapema kuliko kuishi naye ndani pasipo kujua".
Ameongeza kuwa kwa upande mmoja ametutia pengo "Tunashukuru, Hakuna mtu anayefanya maamuzi siku moja hivyo kwa mtulia ni kama alikuwa kwenye uchumba muda mrefu na sasa ameamua kwenda kuoa kabisa au kuolewa".
Chanzo: EATV
