Tanzania itakuwa ya hovyo kuishi - Nape Nnauye

Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh Nape Nnauye amefunguka na kusema kuwa kama nchi ya Tanzania viongozi wa kisiasa hawatajifunza kufanya siasa za kuvumiliana basi nchi itakuwa ya hovyo sana

Nape Nnauye amesema hayo siku moja baada ya kuzikwa kwa mmoja wa Waasisi wa CHADEMA, Mzee Victor Kimesera na kusema kuwa kwake wanajifunza siasa za kuvumiliana 
"Pumzika Mzee Kimesera, kwako tunajifunza siasa za kuvumiliana! Viongozi wa kisiasa tusipojenga Utamaduni wa Kuvumiliana Tanzania itakuwa nchi ya hovyo kabisa kuishi" alisisitiza Nape Nnauye 
Mbali na hilo Nape Nnauye ametoa ujumbe wake wa Pasaka kwa wananchi wake wa Mtama na kuwataka kupendana na kushilikiana kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lao la Mtama na kuhakikisha jimbo hilo linakuwa jimbo la mfano nchini. 
"Sikukuu hii ya Pasaka ikafufue ari ya kuendelea kupendana na kushirikiana katika kuhakikisha jimbo letu linakuwa la mfano nchini, kwa maendeleo , mafanikio , furaha na umoja bila kujali tofauti zetu mbalimbali. Nawatakia Pasaka njema" alisema Nape Nnauye 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo