Mange Kimambi aibukia Tarime vijijini

Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chaha (CHADEMA) ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha polisi kutaka kuzuia mkutano wa Mbunge wa Tarime Vijijini CHADEMA, Mhe. John Heche kwa kile kinachodaiwa kuhofia maandamano yanayoratibiwa na Mange Kimambi

Mara Ryoba amesema kuwa polisi wamekuwa na upendeleo kwa kuwa wanaona watu wa CCM wakiendelea kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa ili hali watu wa upinzani wakizuiliwa. 
"Haki huinua taifa; bali dhambi ni aibu ya watu wote. Nimepata taarifa kwamba Mbunge wa Tarime vijijini Mh. John Heche alizuiliwa asifanye mkutano Sirari eti kisa kuna maandamano ya Mange Kimambi, kwanza maandamano sio dhambi yapo kwa mujibu wa katiba yetu" alisema Mbunge Marwa Ryoba 
Kwa mujibu wa Mbunge wa Tarime Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, John Heche amethibitisha hilo kuwa ni kweli kulikuwa na jaribio la kutaka kuzuiwa kufanya mkutano wake na wananchi wa Sirari kwa hofu ya maandamano ya tarehe 26 mwezi wa nne. 
"Ni kweli polisi walitaka kutuzuia kufanya mkutano ila pamoja na polisi Sirari kufanya jaribio la kutaka kuzuia mkutano wangu na wananchi, kwa kisingizio cha hofu ya maandamano ya tarehe 26. Mkutano wangu ulifanyika na umemalizika salama, Asanteni sana wananchi wa Sirari kwa kujitokeza kwenye mkutano wetu" alisema John Heche.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo