CHADEMA Yazidi Kupoteza, Diwani Mwingine ahamia CCM

Aliyekuwa Diwani wa kata ya Osunyai kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika Halmashauri ya jiji la Arusha ndugu Elrehema Amosi Nniko, ametangaza kujivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake na kujiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivyo kupoteza sifa ya uwakilishi katika kata yake.
Diwani huyo aliyechaguliwa mnamo october mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu, leo Machi 10, 2018 ametangaza rasmi kukihama chama chake na kujiunga na CCM, kwa kile alichodai ni kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Mh. John Pombe Joseph Magufuli.
Mara tu baada ya kufanya maamuzi hayo leo Jumamosi Machi 10, Diwani huyo amepokelewa na Katibu mwenezi wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Arumeru mjini ndugu Abrahamu Molley na Katibu wa hamasa wa vijana mkoa wa Arusha ndgu Omary Lumato.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo