Sisafiri kwenda nje kwa sababu sio jimbo langu - Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa anapokea mialiko mingi kutoka nje ya nchi lakini amesema hawezi kusafiri kwenda huko kwasababu sio jimbo lake.
Ameyasema hayo mapema hii leo mkoani Singida katika uzinduzi wa kiwanda cha kukamua alizeti, ambapo amesema kuwa jimbo lake ni Tanzania hivyo hawezi kusafiri.
Amesema kuwa licha ya kupata mialiko mingi kutoka nchi za nje, hawezi kusafiri mpaka pale atakapoitembelea Tanzania yote na kutatua kero za wananchi.
“Mimi jimbo langu ni Tanzania, ndio maana nalitembelea ili kuweza kutatua kero mbalimbali za wananchi, kwa hiyo siwezi kusafiri kwenda nje,”amesema Rais Dkt. Magufuli
Hata hivyo, Rais Magufuli amewata Wabunge, Madiwani na watendaji kuwatembelea wananchi ili waweze kutatua kero mbalimbali za wananchi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo