Siku moja baada ya kujiuzulu diwani wa Isapulano kupitia
CHADEMA NA kisha akajiunga na CCM Mh Alphonce Mbilinyi, mwenyekiti wa Chama cha
demokrasia na maendeleo CHADEMA Wilaya ya Makete Ibrahim Ngogo amezungumzia
uamuzi wa kiongozi huyo kuhamia CCM na kusema walikuwa mbioni kumtimua
Mwenyekiti huyo amesema walimuita marakadhaa katika chama
chao na kumuonya kutokana na mwenendo wake usioridhisha na akaahidi kuyatendea
kazi maagizo hayo, lakini amejiuzulu kabla ya kikao kingine kilichopangwa
kufanyika Aprili mwaka huu ambacho kilikuwa kimtimue kwenye chama hicho endapo
kusingekuwa na mabadiliko yeyote
Ngogo amesema huwenda diwani huyo amekimbilia CCM kwasababu
aliogopa kutimuliwa kwenye chama chao, na kusema pamoja na yote aliyoyafanya,
uchaguzi mdogo wanaimani CHADEMA itashinda kama uchaguzi utakuwa huru na wa
haki