Imeelezwa kuwa kwa sasa Chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA hakina kiongozi anayeisumbua CCM baada ya kuondoka kwa aliyekuwa katibu
mkuu wa Chama hicho Dkt Wilbroad Slaa ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa balozi
Akizungumza na wajumbe wa UWT na wanachama wa CCM wilaya ya
Makete, Katibu wa UWT Taifa Amina Makilagi amesema chama hicho hakina sera,
kimebaki kupiga kelele tu huku akisema mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe
haiwezi nafasi hiyo ya uenyekiti
Amesema kitendo cha aliyewahikuwa Mbunge wa Singida
Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu Kuhamia CHADEMA ilikuwa ni kukibipu chama cha
Mapinduzi ambacho kimeamua kuweka kifurushi cha Bila kikomo cha kuwakomba
viongozi na wanachama wa upinzani mpaka uchaguzi mkuu ujao 2020
Tazama Video Hii hapa chini:-
