Basi la New Force lilikuwa linatokea Msamvu kwenda Mikese liligongana na gari dogo la abiria (Hiace) lililokuwa linatokea Msamvu, mkoani Mogororo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu watano wamefariki dunia huku wengine 9 wakiwa wamejuruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Morogoro.
Kwa mujibu wa mashahuda wa tukio hilo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa hiace ambaye alikuwa akitaka kulipita gari la mchanga lililokuwa mbele yake hivyo akajikuta amegongana uso kwa uso na basi hilo.
