Tume kuchunguza kupigwa mwalimu na Mwalimu Mwenzake

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Missana Kwangula amesema anatarajia kuunda tume ya kuchunguza tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabwe, Jackson Mussa za kumpiga walimu Emmanuel Mbemba.
Inadaiwa kuwa mkuu huyo wa shule alimshambulia mwalimu huyo kwa kumpiga makofi, ngumi na mateke, kitendo ambacho kilishuhudiwa na wanafunzi wake na jumuiya ya shule hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kwangula alisema kabla ya kuunda tume hiyo ya wataalamu, kwanza atatuma maofisa elimu kutoka Idara ya Elimu ya wilaya ya Nkasi kufuatilia tukio hilo kubaini kilichotokea.
"Maofisa elimu hao kutoka Idara ya Elimu wilayani hapa watakwenda shuleni hapo kufuatilia tukio hilo na kuzungumza na wahusika ili kubaini ukweli wake, ushauri wao unaweza kunipatia mwanga wa nini kilitokea," amesema Kwangula.
Mkuu wa shule hiyo, Mussa anatuhumiwa kumshambulia mmoja wa walimu wake, Mbemba kwa kuchapa makofi, ngumi na mateke baada ya kusisitiza kuwa amwandikie barua ya ruhusa ili aweze kwenda ziara ya mafunzo na wanafunzi wa Kidato cha Tatu kwenye fukwe za Ziwa Tanganyika.
Mbemba anafundisha somo la Jiografia kidato cha tatu katika shule hiyo ya serikali, ambayo ipo katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika katika Kata ya Kabwe wilayani Nkasi.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) wilaya ya Nkasi, Hery Mtovano amesema chama hicho kimemshauri Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Kwangula kumshusha cheo Mussa kwa kosa la kumdhalilisha Mwalimu Mbemba mbele ya wanafunzi wake.

IMEANDIKWA NA PETI SIYAME, NKASI


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo