Ng'ombe akiwa amefungwa kwenye nguzo ya Umeme Makete mjini kama ilivyokutwa na Mwandishi wetu
Shirika la umeme
TANESCO wilaya ya Makete limetoa onyo kali kwa wananchi hasa wafugaji ambao
wamekuwa wakifunga mifugo yao kwenye nguzo za umeme ama kwenye nyaya
zinazoshikilia nguzo hizo
Onyo hilo limetolewa
na Meneja wa TANESCO wilaya ya Makete Bw. Henrico Renatus baada ya mwandishi
wetu kukuta mwananchi mmoja mkazi wa Makete mjini katika Mji Mdogo wa Iwawa
kufunga ng'ombe kwenye waya unaoshikilia nguzo ya umeme
Meneja huyo
amelielezea tukio hilo ambalo lililalamikiwa na baadhi ya wananchi
waliolishuhudia na kukiri kupokea malalamiko hayo lakini hakuwa tayari kumtaja
mwananchi huyo aliyefanya hivyo
Ameelezea hatari
inayoweza kutokea kwa wananchi kufanya vitendo hivyo ikiwemo nguzo hizo kukosa
uimara wake, pamoja na vikombe vinavyobeba nyaya kupasuka na kusababisha waya
unaoshikilia nguzo kusafirisha umeme ardhini na kusababisha madhara makubwa kwa
wananchi
Ikumbukwe kuwa
vitendo vya kuchunga mifugo ovyo katika eneo la miji ni marufuku kwa mujibu wa
sheria licha ya baadhi ya wananchi kuamua kukiuka sheria hiyo na kufunga mifugo
kwenye nguzo za umeme licha ya kuwepo mabango yaliyoandikwa hatari kwa
kumaanisha kukataza mwananchi kufanya chochote kwenye nguzo hiyo

