Shekhe Kundecha amesema hayo wakati akiongea na mwandishi wa habari na kusema kuwa si kila mtu ambaye anakwenda CCM ameridhika na hali hiyo na kudai wapo watu wamekubali kwenda kwa kulazimika kufanya hivyo.
"Siyo kila kukubali ni kuridhika na hilo jambo kuna kukubali jambo kwa kulazimika kufanya hivyo, waswahili wanasema hivi mkono usioweza kuuvunja basi ubusu kwa hiyo akikikuta mtu unaubusu anaweza kusema umeridhika kwamba eti umeshindwa hatua ya kuufanya kwa hivyo kujisalimisha nao una busu tu, sasa si kila kubusu ni kuridhika na hilo jambo kwa hiyo watu wanaweza kuwa wanakwenda kule kwa sababu ya kulazimika hawana hawana njia ya kufanya lakini si ishara ya kuwa watu wanakubali kama unatafakari kwa umakini" alisema Kundecha
Shekhe Kundecha ametoa kauli hiyo wakati ambao viongozi mbalimbali wa CHADEMA na vyama vingine vya siasa nchini wakiwa wamejizulu nafasi zao katika vyama vyao na kujivua uanachama wa vyama hivyo na kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kauli ya kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano na Rais John Pombe Magufuli.
