Mapya Kuhusu Mwandishi wa Habari aliyekamatwa Makambako Njombe


Na Brighiter Nyoni, MAKAMBAKO

Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la EMMANUELI KIBIKI mkazi wa mtaa wa Mwembetogwa Mjini Makambako anayedaiwa kuwa ni wandishi wa habari wa kujitegemea anashikiliwa na shirika la umeme Tanesco wilaya ya makambako kwa tuhuma za kuiandikia barua ya upotoshaji shirika hilo kuwa meneja wa Tanesco Makambako na mkoa wa Njombe wanashirikiana kufanya hujuma za kuharibu miundombinu ya umeme na kulisababishaia hasara  shirika hilo.

Akizungumza na Eddy Blog Kaimu meneja wa wateja wakubwa wa shirika la umeme Tanesco kutoka makao makuu Dar es salaam  FREDRICK NJAVIKE amesema kuwa kutokana na barua hizo ambazo zinaonesha hujuma ndani ya shirika hilo ikiwemo hasara ya kuungua kwa transifomer na kukatika kwa umeme ndizo ambazo zimepelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Aidha Kaimu meneja huyo  amesema kuwa baada ya makao makuu kupata taarifa hizo imewalazimu kuunda tume ya kikosi kazi ambayo imefika Makambako na kupita kwa wateja zaidi ya 950  ili kuibani hilo na kugundua kwamba taarifa hizo zilikuwa ni za upotoshaji na kwa hali iyo imeisababishia shirika hilo kupata harasa kubwa kutokana na uundwaji wa tume hiyo ya uchunguzi.

Kwa upande wa mke wa Emmenuel Kibiki, Bi TOBINA MPOGOLO amesema kuwa mumewe kwa sasa siyo mwandishi wa habari tena kwa kuwa aliachana na taaluma hiyo baada ya kuanza kusomea masuala ya sheria mwaka 2009.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo