Mtatiro amesema hayo na kudai kuwa huenda kuna mpango wa kutaka kumkabidhi ofisi hiyo Mwenyekiti wa CUF ambaye anatambulika na Msajili wa vyama vya siasa nchini Profesa Lipumba na kudai wao wanaendelea kufuatilia kujua nini kimewapeleka pale polisi.
"Polisi wakiwa na magari kadhaa, wameivamia Makao Makuu ya Chama cha Wananchi CUF Mtendeni, Zanzibar saa 12.10 jioni hii. Inaonekana/inahisiwa wana ajenda mbili; moja ni kuikalia makao makuu hiyo kimabavu ili kesho Jumatatu waikabidhi kwa Bwana yule ili kutekeleza mkakati maalum, au wana lengo la kuingia kimabavu na kuweka vitu hatari na kisha kuwakamata viongozi wa CUF na kudai walitunza vitu hatari ofisini hapo. Tunafuatilia jambo hili kwa ukaribu " Julius Mtatiro


Polisi wakiwa na silaha wamevamia Makao Makuu ya CUF katika mtaa wa Mtendeni, mjini #Zanzibar tokea saa 12 jioni. Haijafahamika ni nini malengo yao. pic.twitter.com/jWBP1oDqDb— Ismail Jussa (@IsmailJussa) February 18, 2018
