Kijiji cha Ilevelo
wilayani Makete Mkoani Njombe huwenda kikakumbwa na upungufu wa chakula msimu
huu, kutokana na ongezeko la Ngedere wanaoharibu mazao katika mashamba ya
chakula yaliyolimwa na wananchi hao katika kijiji hicho
Wakizungumza na mwandishi wa Green
Fm wananchi hao wamesema wanyama hao waharibifu wanazidi kuongezeka katika
kijiji chao kila kukicha ambapo kwa sasa wanaharibu mahindi na Njegere
mashambani
Edson Sanga mkazi wa
kijiji hicho amesema tatizo hilo ni kubwa lakini kwa kiasi kikubwa limechangiwa
na upandwaji miti hadi kwenye mashamba yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo hivyo
hata ufukuzaji wa wanyama hao umekuwa mgumu
Naye Bibi Sikujua
Sanga amesema anaziona dalili za njaa katika kijiji chao huku akiiomba serikali
kuchukua hatua zaidi katika utekelezaji wa agizo la kuondolewa miti ya mbao
kwenye mashamba ya kilimo
Mwenyekiti wa kijiji
cha Ilevelo Bw. Seso Mahenge amezungumzia suala hilo na kusema Wao kama Kijiji
hawajakaa kimya kukabiliana na tatizo hilo
Pia amesema
wanapeleka ombi lao katika idara husika iliyopo halmashauri ya wilaya ya Makete
kuomba msaada zaidi wa kuwafukuza wanyama hao ili kuepuka madhara
yatakayowapata wananchi wake ambao wengi wao wanategemea mazao waliyoyalima
shambani kujikimu kimaisha



