Katika kupambana na watumiaji na wasambazaji wa dawa za kulevya pamoja na pombe za kienyeji Kituo cha polisi Mwera kimefanikiwa kuwakamata watu 6 wakiwa na lita 720 za maroweko ya pombe za kienyeji.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharib Unguja Hassan Nassir ali amesema vijana hao wanajiita mbwa mwitu walikamatwa huko Ndunduke wakiwa na lita 720 za maroweko ya pombe za kienyeji, Matangi 7 pamoja na Mbwa wao 14.
Vijana hao ni Omar Haji Makame (20) na Rashid Kheir Haji (19) wa Mtoni Kidatu , Hassan Haji Moh’d (18) na Ali Mzee Othman (20) wa Kwamtipura, Silima Bakari Silima (18), na Sleimani Juma Ali(29) wa Shaurimoyo.
Kamanda Nassir amesema wamegundua kuwa Ndunduke ndani ya eneo la msitu wa Masingini kumegeuzwa maficho ya wahalifu hivyo watahakikisha vijana hao wanaeleza matukio yote ya kiuhalifu yanayofanyika na kusema watawapiga risasi Mbwa waliowakutanao kutokana na ushahidi kuonesha kuwa Mbwa hao walikuwa wakitumika kihalifu kwa kuwakamata raia wema na kuwapora mali zao.
