Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Kagera wilaya ya Muleba katika kata ya kasindaga wakati wa uzinduzi wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa mkoani humo
Waziri Nchemba amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani wake kisha nikuwaambia wananchi nini kinachoendelea.
"Mataifa mengine mtu akiuwawa shighuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu wanapote potea kama mtu kapuliza dawa ya mbu, kama jambo la kawaida tu, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili". amesema Waziri Mwigulu
Ameongeza kusema kuwa maswala ya demokrasia huamuliwa kwa peni na karatasi na si kwa panga, rungu wala mkuki na kila mtu anayo haki ya kuwa katika chama chochote cha siasa nchini.
Katibu Daniel John aliuawa kwa kukatwa mapanga baada ya kuamriwa kuingia kwenye gari na baadaye mwili wake kuokotwa kwenye ufukwe wa 'Coco Beach' ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali.