Mambosasa amesema hayo leo Februari 16,2018 wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya jeshi hilo kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu akiwepo dereva wa basi, kondakta na kijana mwingine ambaye ni mlemavu wa miguu wakituhumiwa kukutwa na bangi.
"Tumekamata keti 491, ndoo mbili za ujazo wa lita 20 zikiwa zimejazwa bangi ndani baada ya kuendelea na uchunguzi tukakuta ndoo mbili zenye ujazo wa lita 10 zikiwa zote zimejazwa madawa ya kulevya aina ya bangi na walikuwa wameziweka kwenye buti la basi hilo. Watuhumiwa ambao wamekamatwa kwenye basi hilo ni Shaban Said (52) yeye mkazi wa Manzese ni dereva wa basi hilo pia alikamatwa Omari Juma (27) yeye ni kondakta na mwisho alikamtwa Hashim Mohamed (42) watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa watafikishwa punde mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika" alisema Mambosasa
Mambosasa aliendelea kutolea ufafanuzi sakati hilo kwa kumuinua kijana mmoja ambaye ni mlemavu wa miguu ambaye yeye ndiye inasemekana mmilki wa mzigo huo wa bangi ambao umekamatwa na jeshi la polisi.
"Huyu sasa ndiye mmiliki wa madawa haya mnaweza kuona mtu wa kumuonea huruma sasa ndiye anauwa Watanzania yaani tunapambana na vita ya madawa ya kulevya lakini huyu comrade ndiye mfanyabiashara wa madawa hayo, niendelee kusema hakuna atakayeachwa kwa aina yoyote ile kuendelea kuvunja sheria, sisi hatuangalii mtu ila tunaangalia kitu anachokifanya na tutakwenda mbali zaidi kuchunguza kama mmiliki wa basi na yeye anaendelea kurusu mabasi yake kubeba madawa ya kulevya"