Mbaroni kwa kuvamia kituo cha polisi

Watu wawili wamekamatwa na wengine wawili wakidaiwa kutoroka baada ya Jeshi la Polisi wilayani Ruangwa mkoani Lindi kufanikiwa kuwatia mbaroni kwa madai ya kutaka kuvamia kituo cha polisi wilayani humo huku wakiwa na silaha za kivita

Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga amesema kwa sasa watu hao wako chini ya ulinzi na wanaendelea kuhojiwa.
Amefafanua kwamba “Watuhumiwa hao walikuwa wakizunguka kituo cha polisi kabla ya kudhibitiwa na baadaye kufuatiliwa na kukutwa na zana hizo mbalimbali za uhalifu.” Kamanda Mzinga.
Pamoja na hayo imebainishwa kwamba katika msako ulioendeshwa wilayani Liwale, Polisi wamefanikiwa kukamata silaha ikiwemo bunduki moja ya SMG na mapanga matatu pamoja na vifaa mbalimbali vya kuvunjia sanjari na risasi.
Hata hivyo Jeshi la polisi mkoani Lindi limeendelea kuitahadharisha jamii kutojihusisha na masuala ya  uhalifu huku ikiwekw wazi kwamba taarifa kamili juu ya watuhumiwa itatolewa baada ya kukamilika kwa upelelezi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo