Mahakama yaamuru ‘Nabii Tito’ akapimwe Mirembe

Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka katika taasisi ya magonjwa ya akili mshtakiwa Onesmo Machibya maarufu Nabii Tito, ili kujua iwapo ana akili timamu au la.

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, James Karayemaha ametoa agizo hilo leo Jumatatu Februari 19,2018.

Amesema Magereza wanachelewesha haki ya mshtakiwa na kwamba, anashangaa ni kwa nini wanashindwa kutekeleza agizo la kumpeleka kufanyiwa uchunguzi.

"Naagiza amri ya Mahakama itekelezwe, apelekwe taasisi ya magonjwa ya akili Isanga (Mirembe) si kama alivyoleta vielelezo kutoka Muhimbili," amesema Karayemaha.

Hakimu ameahirisha kesi hadi Machi 5,2018 itakapotajwa kwa ajili ya kupokea taarifa ya uchunguzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo