Mange Kimambi asababisha Polisi Kuchukua Hatua Hii

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Muliro J. Muliro amefunguka na kusema kuwa wamemchukulia hatua za kinidhamu askari polisi wake mmoja ambaye jina lake halijawekwa wazi kufuatia kuonekana akichukua rushwa kwenye video za mitandaoni

Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja masaa kadhaa baada ya Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, mrembo Mange Kimambi kuposti video ya askari polisi akichukua rushwa ya pesa kutoka kwa raia ambaye alitenda kosa la barabarani.
Akithibitisha juu ya kuchukua za kinidhamu kwa askari huyo Kamanda Muliro amesema ni kweli Jeshi la Polisi limechukua maamuzi hayo kwa askari huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake. 
"Ni kweli tumechukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria na kanuni za kipolisi kwa askari yule, kuhusu jina lake kwa sasa hatuwezi kuliweka wazi kwa kuwa jeshi la polisi haliwezi kufanya kazi kwa matangazo" alisema Muliro 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo