Mambosasa: Asije kujutia kwa yatakayotokea kwani jeshi limejipanga vilivyo

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es salaam limewaonya wananchi ambao wanaojiandaa na maandamano yanayoratibiwa kupitia mitandao ya kijamii na kusema kwamba wasijaribu kufanya hivyo kwani wataingia kwenye matatizo makubwa

Akizungumza na leo na waandishi wa habari Kamanda Mambosasa amesema kwamba Watanzania wajiepushe na uchochezi huo wa watu wachache wa kutaka kuiingza nchi kwenye vurugu.
Aidha Mambosasa amesema kwa yeyote ambaye hatasikia onyo hilo kwa mkoa wa Dar es salaam asije kujutia kwa yatakayotokea kwani jeshi limejipanga vilivyo na kwamba kwa sasa liipo kwa ajiili ya kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji.
"Kuna watu ambao wanaendelea kuhamasisha wananchi kuvunja sheria. Wanataka wajiandae kwa maandamano, tarehe wanazoendelea kutaja.  lakini wanafanya hivyo wao wakiwa wamekaa sehemu salama. Wanataka kuwaingiza watanzania wengine kwenye shida,". Mambosasa.
Kumekuwa na vuguvugu la kufanyika maandamano  Aprili 26 huku Mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi akionekana kuwa mstari wa mbele katika uhamasishaji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo