IGP Sirro atoa Onyo Kali kwa wanaotaka Kuandamana

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewaonya wanasiasa ambao wamepanga kuandamana nchi nzima kwani jeshi lake limejipanga kukabiliana nao.
Akizungumza jana mkoani Simiyu Jumatatu Februari 26, IGP Sirro amesema kuwa jeshi hilo limepata taarifa kutoka katika vyanzo vyake juu ya kuwepo kwa makundi ya vijana ambao wanajiita Wanamapinduzi waliopanga kuandamana nchi nzima chini ya uratibu wa chama kimoja cha siasa ambacho hakukitaja.
“Yeyote atakayeandamana au atakayebainika akiwa katika mikakati ya maandamano atashughulikiwa sisi wamejipanga kikamilifu kukabiliana na wandamanaji ikiwa ni pamoja na kuwakamata watu wote watakaoandamana.
“Tumeshapata taarifa kuwa kuna vijana wanajipanga kuandamana nchi nzima sisi kama jeshi la polisi tumejipanga vyema kuhakikisha tunawadhibiti wasiweze kufanya chochote  na mtu yoyote ambaye ataandamana tutamchukulia hatua za kali za kisheria,” amesema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo