Mkutano wa Mh. Zitto wavamiwa na polisi

Mkutano wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya Defender

Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Chama hicho, imeeleza kuwa polisi baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi.
Taarifa kwa waandishi
MKUTANO wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo,ndugu Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya defender
.Baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji Taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani Wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi
Abdallah Khamis
Afisa Habari
ACT Wazalendo
26/02/2018
Zitto yupo katika ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo