CHADEMA: Makao Makuu ya chama Chetu Yamevamiwa Leo

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA
POLISI WAMEVAMIA MAKAO MAKUU YA CHAMA KINONDONI.


Leo Jumatatu tarehe 19 Februari, 2018 majira ya saa moja Kamili jioni hii Polisi waliokuwa na Magari matano walivamia ofisi za Makao Makuu ya Chama Kinondoni na kuwakuta walinzi na kujitambulisha kuwa wametoka kwenye ofisi za Upelelezi Kanda Maalum ya DSM .
Polisi hao waliwajulisha walinzi wetu kuwa wanataka kufanya upekuzi kwenye ofisi zetu pamoja na kuwa hawakuwa na hati ya upekuzi na wala hawakuambatana na viongozi wa Serikali ya Mtaa kama ambavyo sheria inawataka. Aidha, tunatambua kuwa Sheria inawataka Polisi kupekuliwa kwanza kabla ya kuanza zoezi hilo.
Walinzi wetu waliwakatalia kwa kuwa hawakufuata utaratibu na wala hawakueleza kuwa wanataka kupekua nini ndani ya ofisi zetu.
Tunalaani kitendo hiki na tunajiuliza kwanini wamekuja usiku ? Na ikiwa ni siku moja tuu baada ya polisi kufanya uvamizi kama huo kwa Chama Cha CUF Zanzibar na kufanya upekuzi Jana usiku.

Je? Huu ndio utaratibu mpya wa Jeshi la Polisi kwa Vyama vya Siasa ?
Tunatoa mwito kwa Jeshi la Polisi kuwa wafuate Sheria za nchi katika kutimiza wajibu wao kwani ni jambo la hatari kwa wasimamizi wa Sheria kuvunja Sheria wanazopaswa kuzisimamia.
Tutaendelea kutoa taarifa kadiri tutakavyozipata.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Imetolewa Leo Jumatatu tarehe 19 Februari 2018


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo