Yanga SC yalicharukia gazeti la michezo nchini kwa kosa hili

Klabu  ya soka ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wake wa makundi nchini umelaani vikali kitendo cha muandishi wa habari wa gazeti la Mwanaspoti kuandika mashabiki wa Simba SC kupitia mitandao ya kijamii wamempa pole Kocha Lwandamina kwa msiba wa mwanae pamoja na kumpatia ubani wa Tsh. 3 milioni badala ya Yanga SC

UPOTOSHWAJI WA MAKUSUDI ULIOFANYWA NA GAZETI LA MWANASPOTI LA LEO JUMATATU 15/01/2018
KATIKA HABARI ILIYOPO UKURASA WA PILI IKIWA IMEANDIKWA NA MWANDISHI KHATIMU NAHEKA.
Aya 3 za Mwisho ameandika “Mashabiki mbalimbali wa Simba kupitia mitandao ya kijamii. siku ya Jumamosi Wamempa pole Kocha Lwandamina kwa msiba wa mwanae pamoja na kumpatia Ubani wa Tsh. 3 milioni.”
KITU AMBACHO SI KWELI.
Huku ni kuwakosea heshima mashabiki wa Yanga ambao kwa umoja wao ndiyo waliompa kocha wa timu yao pendwa Ubani huo, kupitia michango ya group za WhatsApp.
Nichukue nafasi hii kuwaomba wanayanga wote kulaani vikali upotoshwaji huu wa makusudi wenye lengo la kuchafua heshima ya klabu,wanachama na mashabiki wa Yanga.
By Robert Kasela
Mwenyekiti
Umoja wa Group za Yanga.




JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo