CCM kuibomoa UKAWA Dar es Salaam

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejipanga kuhakikisha kinarejesha Kata mbalimbali kilizopoteza na kuchukuliwa na vyama vya upinzani katika jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa kwa sasa wanajipanga kuhakikisha Kata pamoja na mitaa waliyopoteza inarudi.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi wakati akiongea na waandisha wa habari amedai kuwa kwa sasa wameanza kuondoa changamoto mbalimbali ndani ya chama hicho kuhakikisha wanashinda na kukomboa mitaa na Kata ambazo zipo chini ya wapinzani. 
"Tutahakikisha katika changuzi zozote zilizopo mbele yetu kama ule wa Saranga uchaguzi mdogo ni kuhakikisha tunarudisha mitaa iliyobaki na Kata zilizobakia" alisisitiza Mbaruku 
Katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika Novemba 26, 2017 uliwapa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Saranga Ubungo na kuweza kukomboa Kata hiyo ambayo awali ilikuwa chini ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo