Wizara ya Elimu yatoa tamko

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia imewataka watanzania wote nchini waliopoteza vyeti vyao vya elimu watoe taarifa mapema katika sehemu husika na wasisubiri mpaka pale wanapokuwa na uhitaji navyo ndio waanze kuhangaika

Hayo yameelezwa leo (Jumatano) Bungeni na Naibu Waziri Wizara ya hiyo Mhe. William Ole Nasha kwa niaba ya Waziri ya Waziri Sayansi, Teknolojia wakati alipokuwa anajibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato David Chumi ambapo alitaka kufahamu serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu ina mpango gani wa kuwasaidia watanzania waliopoteza vyeti vyao vya elimu na kuvipata vingine.
"Muhitimu aliyepoteza cheti hupatiwa cheti mbadala au uthibitisho wa matokeo kwa kufuata taratibu zilizowekwa kama kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi, kutangaza gazetini na endapo cheti hakikupatikana hata baada ya kukitangaza katika vyombo vya habari basi muhitimu atahitajika kujaza fomu maalumu",alisema Mhe. William Ole Nasha.
Pamoja na hayo, Mhe. William Ole Nasha aliendelea kwa kusema "natoa wito kwa wananchi kuwa iwapo umepoteza cheti cha masomo, anza taratibu za kuomba cheti mbadala, usisubiri mpaka unapokuwa na uhitaji ndipo uanze taratibu za kuomba".
Kwa upande mwingine, Mhe. William Ole Nasha amesema muombaji wa cheti mbadala au uthibitisho wa matokeo hupatiwa huduma baada ya kumaliza utaratibu wote uliyowekwa na Wizara hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo