Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akizungumza na wananchi wa Utweve Makete
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy akizungumza kwenye Mkutano huo
Mwananchi akitoa kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka
amesema atafuatilia hatma ya mauaji ya mtoto Fedi Atu Sanga (17) anayedaiwa
kuuawa kwa kipigo mwaka 2016 katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani
Makete
Ameyasema hayo baada ya kusikiliza kero za
wananchi wa kijiji hicho hii leo, ambapo pamoja na mambo mengine wananchi hao
wamesema hawaelewi namna kesi hiyo ilivyoendeshwa mpaka watuhumiwa hao
wakaachiwa huru
Hali hiyo ikamfanya mkuu wa mkoa kuchukua maamuzi
ambayo yameonesha kuwaridhisha wananchi wa kijiji hicho Kwa kumuagiza
mwakilishi wa mkuu wa polisi katika ziara hiyo kuwasiliana na viongozi wake
wampelekee nyaraka za kesi hiyo Ikonda
Akizungumza na wananchi, Mkuu wa mkoa
amewahakikishia kuwa hatma ya kesi hiyo itajulikana kwa kuwa wao kama serikali
watahakikisha sheria inafuatwa
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amewataka
wananchi wa wilaya ya Makete kuanza kujenga utaratibu wa kuwafanyia tohara
watoto wao wa kiume wakiwa wadogo kama njia mojawapo ya kupunguza kiwango cha
maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi
Sikiliza sauti hizo hapo chini:-





