Madiwani watatu CHADEMA wasimamishwa

Madiwani watatu wa CHADEMA halmashauri ya Mji wa Njombe wametolewa nje ya kikao cha baraza la madiwani na kusimamishwa kuhudhuria vikao 3 kutokana na kujadili mkataba wa halmashauri na kampuni iliyowekwa kukusanya ushuru ambayo inawanyanyasa wananchi

Madiwani hao ni pamoja na George Sanga diwani Kata Ramadhani, Sigrada Mligo, diwani viti maalum, Legnard Danda, diwani kata Ihungilo ambao walitolewa kwenye mkutano na kusimamishwa kuhudhuria vikao vitatu baada ya kuhoji mkataba wa halmashauri na kampuni ya Ihagara inayo kusanya ushuru mjini Njombe ambayo inadaiwa kuwanyanyasa wananchi. 
Awali Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga alipiga marufuku kujadili suala hilo kwa madai kuwa baraza halina mkataba huo na hakuna palipo andikwa jina la kampuni hiyo.
"Ihagala kama nani? Tumewaambia sisi hatujamwajiri na baraza hili halijamwajiri huyo Ihagala hivyo sisi tunamjadili kama nani? Nimewaambia hayo mapendekezo yote wayapeleke kwa Mkurugenzi yeye ndiye mwajiri wa Ihagala" alisema Mwanzinga 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo