Waziri Mpya alieteuliwa na Rais Magufuli leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 06 Januari, 2018 amemteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.
Mhe. Doto Mashaka Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na  alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.
Kufuatia uteuzi huu Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Naibu Mawaziri wawili.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.
Mhe. Doto Mashaka Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe 08 Januari, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Januari, 2018


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo