Jeneza lenye mwili likipelekwa msikitini.
Mwili ukifikishwa msikitini.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa nyumbani kwa marehemu Sinza Madukani.
Msikiti ambapo mwili huo umefanyiwa dua kabla ya mazishi.
Safari ya msikitini.
Mashehe wakiomba dua.
Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari makaburini hapo.
RAIS Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza mamia ya waombolezaji katika kuaga na kuuzika mwili wa aliyekuwa mpiga picha wa magazeti ya Serikali, Athumani Hamisi Msengi ambaye amezikwa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisalimiana na waombolezaji.
Msengi alifariki jana Januari 4, 2017 asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Wanahabari na waombolezaji wakiwa makaburini kwa ajiri ya maziko hayo
Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Msengi.
Waombolezaji wakiweka mchanga kaburini.
Shughuli ya mazishi ikiendelea.Picha na GPL