Ule Mchakato wa Muda Mrefu Waiva, Meya Isaya Mwita atoboa Siri

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa tayari wameshakamilisha mchakato wa upatikanaji wa Mwenyekiti na wajumbe wa bodi wa Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam (DDC) na kwamba wakati wowote majina hayo yatatangazwa.

 Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa leo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa mchakato wakuteua wajumbe huo ulishakamilika na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni mashauri yano.

Aidha mbali na hilo, lakini pia alisema kuwa kabla ya kutangazwa kwa majina hayo ,hufikishwa kwa rais na baada ya hapo hutolewa kwa wananchi na hivyo kujua wajume ,mwenyekiti wa bodi hiyo.

Taarifa hiyo ya Mstahiki Meya Mwita imekuja baada ya wajumbe wa baraza hilo kutaka kufahamu hatua lizofikiwa katika mchakato mzima wa uteuzi wa majina ya Mwenyekiti, wajumbe wa bodi ya DDC.

 " Napenda ieleweke kuwa mchakato wa kupata wa jumbe wa bodi ya DDC ulishakamilika, unakwenda vizuri, na muda wowote wananchi wa jiji la Dar es Salaam mtapewa taarifa kupitia vyombo vya habari , kilichofanyika ni kupendekeza majina ambayo tayari kazi hiyo imeshafanyika.

Na majina hayo kuyawasilisha kwa rais Dk. John Magufuli,ambapo baada ya kuyatapitia tutayatangaza kwa wananchi na nyie wajumbe pia mtafahamishwa. "alisema Meya Mwita.

Aidha alisema kuwa mchakato huo haufanyiki kwa DDC pekee bali hadi jengo la Machinga Complex ambapo pia utaratibu huo umefanyika kama ilivyo kwenye bodi ya DDC.

Hata hivyo alisema halmashauri ya jiji imeweza kutekeleza miradi iliyopangwa kwa asilimia 95 na hivyo kuwaomba wajumbe wa baraza hilo, kuendelea kuonyesha ushirikiano ili jiji liweze kusonga mbele.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo