Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kusema kuwa anawajua viongozi wanne ambao ni vigogo kuwa wameshiriki katika kupanga mauaji ya mhamasishaji wa utalii nchini Wayne Lotter
Kigwangalla amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari akiwa katika jengo la Swagaswaga House Makao Makuu ya nchini mjini Dodoma wakati akizungumzia juu ya masuala mbalimbali yanayohusu wizara hiyo na masuala ya utalii.
Kufuatia kauli hiyo Waziri kigwangalla amevitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinawakamata vigogo hao mapema iwezekanavyo na kuwa kama hawatafanya hivyo basi yeye atafikisha taarifa kwa Rais John Pombe Magufuli.
Mbali na hilo Waziri Kigwangala Pia amesema katika kipindi cha siku 100, Wizara yake imebaini mitandao 74 ya watu wanaojihusisha na ujangili ikiwa na washiriki 949.
Mwaka jana mwanaharakati wa kuhifadhi Wanyamapori raia wa Afrika Kusini, Wayne Lotter, alipigwa risasi na kuuawa maeneo ya nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam na watu wasiojulikana.
