Mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Azam FC na Yanga utachezwa saa 10 jioni Azam Complex Chamazi badala ya saa 1:00 usiku kama ulivyokuwa umepangwa awali.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema mchezo huo utachezwa siku ile ile ya Jumamosi Januari 27 mwaka huu, bila ya kutaja sababu za kubadilisha muda huo.
Viingilio kwenye mchezo huo utakaokuwa LIVE kupitia channel ya Azam Sports 2 ni shilingi elfu kumi (10,000) kwa jukwaa kuu na shilingi elfu saba (7,000) kwa majukwaa ya kawaida.
Waamuzi wa mchezo huo wote ni kutoka Dar es Salaam ambapo muamuzi wa kati atakuwa ni Israel Nkongo akisaidiwa na muamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na mwamuzi msaidizi namba mbili Soud Lila.
Mwamuzi wa akiba Elly Sasii wakati kamishna wa mchezo huo ni Omar Abdulkadir.
