INAUMA SANA: PICHA JINSI ALBINO ALIVYOUAWA KINYAMA HUKO SIMIYU

Mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) mkazi wa kijiji cha Gasuma kata ya Nkololo wilayani bariadi mkoani Simiyu ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ambao wametoweka na viungo vyake.

Kamanda wa polisi mkoani wa Simiyu Charles Mkumbo amesema tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa marehemu, ambapo wahusika, baada ya kufanya mauaji hayo walimkata mguu wake wa kushoto, sehemu ya goti, vidole 2 vya  mkono wa kushoto pamoja ukucha wa kidole gumba kisha kutoweka navyo.

Chanzo cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni imani za kishirikina na kwamba tayari watu wawili ambao ni waganga wa kienyeji  wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.

TAARIFA KAMILI KUHUSU TUKIO HILI ITAKUIJIA.
 
picha na GPL
 
chanzo: Malunde1 Blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo