Baraza la madiwani wa
halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe linatarajia kuunda tume ya
kuchuguza suala zima la Mapato ya halmashauri hiyo
Hatua hiyo inatokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kutopelekwa kwa wakati asilimia 10 za fedha za vijiji,
pamoja na kupungua kwa mapato ya halmashauri kutokana na sababu mbalimbali
zinazoelezwa na wataalamu pamoja na waheshimiwa madiwani
Baadhi ya madiwani
wakizungumzia hoja ya makusanyo ya halmashauri katika baraza la madiwani hii
leo, wametoa maoni yao ikiwemo kupendekeza utaratibu uliokuwa ukitumika
mwanzoni wa watendaji kupeleka mapato urudishwe ili iwe rahisi kupatiwa
asilimia za vijiji
Mweka hazina halmashauri ya
wilaya ya Makete Edward Mdagachule amelazimika kutolea ufafanuzi hoja hizo
ikiwemo kutopelekwa asilimia 10 za vijiji ambapo amesema mpaka sasa deni
wanalodaiwa na vijiji ni Zaidi ya shilingi milioni 92 huku akitaja sababu za
kutokulipa kuwa ni kutokana na mapato kuwa madogo kuliko matumizi
Amesema fedha zinazopatikana
zimetumika kulipia posho za madiwani, mishahara ya watumishi wanaolipwa kutoka
vyanzo vya mapato ya halmashauri, kununua mashine za makusanyo ya mapato (POS)
37, kulipia timu mbalimbali za uchunguzi, kulipia shughuli mbalimbali za
utawala, pamoja safari za watendaji wa halmashauri
Hali hiyo ikamfanya mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa kudhamiria kuunda tume ya
uchunguzi itakayofanya kazi kikamilifu kuhakikisha suala la mapato ya
halmashauri linarejea katika mstari wake
sikiliza sauti hii
sikiliza sauti hii