Mtoto wa miezi 8 abakwa

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 28 anashikiliwa na polisi nchini India kwa kumbaka mtoto wa miezi 8 ambaye ni binamu yake, na kumsababishia majeraha makali yanayohatarisha usalama wake huko Shakurbasti kaskazini Magharibi mwa mji wa Delhi

Taarifa kutoka nchini India zinasema kwamba mama wa mtoto huyo alikuwa ameenda kazini na kumuacha na wifi yake ambaye ndiye alitakiwa kumuangalia, lakini alichukuliwa na binamu yake aliyesema anakwenda naye chumbani kucheza naye, na kisha kumfanyia kitendo hiko cha kikatili.
Baada ya kurudi kazini mama wa mtoto huyo alimkuta mtoto wake ana damu mwilini huku akilia na sehemuzake za siri kuonekana zimevimba, ndipo alipoamua kumkimbiza hospitali, na baada ya vipimo mtoto huyo alionekana amebakwa na kujeruhiwa.
Kijana anayehusika na tukio hilo ambaye ni ndugu yao wanayeishi naye nyumba moja alikimbia, lakini polisi walifanikiwa kumkamata na kukiri kufanya tukio hilo.
Mtoto huyo bado yuko katika hospitali ya Kalawati Saran anakoendelea kupatiwa matibabu, huku madaktari wakisema kwamba hali yake bado ingawa yuko salama.
Source 
The Times of India


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo