Halmashauri ya wilaya ya
Makete imesema haiwezi kuwa tofauti na agizo la Rais Dkt John Magufuli la
kukataza michango ilihali serikali inatekeleza elimu bure
Hayo yamesemwa na Afisa elimu
msingi wilaya ya Makete Mwl Anthony Mpiluka wakati akitola ufafanuzi hoja ya
michango katika baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete
Amesema katika suala la
michango wananchi wenyewe ndio watumie busara kukubali kuchanga kwa hiari yao
au wakatae kwa sababu hakuna mtu wa kuwalazimisha
Pia amtumia nafasi hiyo
kuwashauri wananchi wa kata ya Lupalilo wilayani hapa kufikiria namna ya
kujenga shule nyingine ya msingi baada ya shule ya sasa kuwepo katika hifadhi
ya barabara hivyo itabomolewa kupisha ujenzi wa barabara ya lami kutoka Makete
hadi Njombe
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Mh Egnatio Mtawa ametaka tafsiri Zaidi itolewe kwa wananchi kuhusu tamko la
Rais Magufuli ili lieleweke kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu kwa wilaya
ya Makete
Msikilize akifafanua
Msikilize akifafanua
