Baraza la usimamizi wa mazingira NEMC limekifungia kiwanda cha kutengeneza lami cha SKOL kilichopo salasala jijini Dar-es-Salaam kutokana na kutokidhi viwango ikiwa pamoja nakutokuwa na kibali cha mazingira pamoja na kutimua vumbi na kuathiri wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho mkuu wa ukaguzi na ufuatiliaji NEMC Dr.Yoana Mtoni amesema pamoja na kukifungia kiwanda hicho ambacho kilikuwa kinakiuka agizo la serikali mara kwa mara pia kimetozwa faini zaidi ya shilingi milion hamsini ikiwa pamoja na kutoa amri ya kuhamisha mitambo yake eneo hilo ili kupisha wananchi waliozunguka kiwanda hicho.
Kwa upande wao wananchi wanaoishi maeneo hayo wameiomba serikali kuchukuwa hatua hasa kwa wawekezaji wanaokiuka utaratibu kwa kuwa kiwanda hicho kilikuwa kikitimua vumbi jambo ambalo linalopelekea kupata magonjwa mbalimbali mara kwa mara.