"Dawa ya Muhuni ni kuwa Muhuni zaidi" - Ole-Sosopi

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, BAVICHA, Patrick Ole- Sosopi amekiri kuwa Chama chake kimeamua kurudi kwenye uchaguzi mdogo haswa wa Kinondoni na Siha kwa kuwa wagundua dawa ya muhuni ni kuwa muhuni zaidi

Akizungumza kwenye Kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa Kinondoni Salum Mwalimu Ole-Sosopi amesema kwamba kilichowafanya kususia uchaguzi mara ya kwanza ni kwamba hakukuwa na faida kubwa ya kupatikana kiongozi kwa wananchi wasio na hatia kwa kumwaga damu.
Ole-Sosopi amesema kwamba baada ya kususia uchaguzi ambao uligomewa kupelekwa mbele sasa wagundua kuwa "dawa ya muhuni ni kuwa muhuni zaidi hivyo ifahamike na iwekwe rekodi kuwa CHADEMA tumerudi na kushiriki na kufanya uchaguzi".
Mbali na hayo Ole-Sosopi ameongeza kuwa hataki chama chake au kingine kisipendelewe bali waachwe wabishane kwa hoja na mwishowe wananchi waachiwe kufanya maamuzi.
CHADEMA walitangaza kugomea uchaguzi mdogo uliofanyika January 13 kwa madai mbalimbali ikiwepo kufanyia hujuma za wazi katika uchaguzi uliofanyika Novemba 26 huku tume ikilalamikiwa kutofanyia kazi malalamiko hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo