Licha ya Kufungwa na Yanga, Azam yapigwa faini, yaombwa ushahidi

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa ligi kupitia kwa Afisa Mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura imetangaza kuipiga faini ya shilingi laki 5 klabu ya Azam FC

Wambura amesema kamati baada ya kupokea ripoti ya  mechi namba 103 kati ya wenyeji Majimaji FC dhidi ya Azam FC timu ya Azam FC iligoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kitndo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu.
Mbali na faini hiyo klabu hiyo pia imetakiwa kuwasilisha ushahidi kuhusu malalamiko yake kwenye mchezo huo ambapo ilidai kutoingia kwenye vyumba hivyo kwasababu vilikuwa vimepuliziwa dawa ambayo ilikuwa inatoa harufu kali.
Kwa upande mwingine mwamuzi wa leo kwenye mechi ya Azam FC dhidi ya Yanga Israel Nkongo ameundiwa kamati ya watu watatu kwaajili ya kuchunguza maamuzi yake kwenye mchezo namba 100 kati ya Tanzania Prisons dhidi ya  Mbeya City kutokana na kuwepo kwa utata katika maamuzi yake.
 Hata hivyo Azam FC Jumatatno iliyopita waliwasilisha barua TFF wakiomba kubadilishwa mwamuzi ili achezeshe mwingine badala ya Israel Nkongo lakini ombi lao limetupiliwa mbali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo