Chidi Benz akamatwa tena na dawa za Kulevya huko Dodoma

Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz anashikiliwa tena  na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na hii inakuwa mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili

Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP, Giless Muroto amesema kwamba ni kweli msanii huyo alikamatwa na taarifa kamili zitatolewa hapo kesho.
Kamanda Muroto amesema "Ni kweli Chidi Benz mnamo tar 30/12/2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zidhaniwayo kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani"
Aidha ameongeza kuwa watuhumiwa wote bado wako mahabusu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo