Mzee Kingunge: Mimi mnanifanyia hivi Lissu mmemfanyaje?

Mwanasiasa mkongwe , Kingunge Ngombale Mwiru ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili kufuatia kung'atwa na mbwa amemkumbuka na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amesafirishwa na kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi

Kigunge amemjulia hali Tundu Lissu baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akiwa amefuatana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati Kuu Mhe. Edward Lowassa walipomtembelea leo Januari 8, 2018 katika hospitali ya Muhumbili. 
"Vipi kuhusu Tundu Lissu? Nimeona mimi jinsi wanavyonifanyia hapa (madaktari) nimewauliza mimi tu niliyeng'atwa na mbwa mnanifanyia hivi Lissu mmemfanyaje maana majeraha yake yalikuwa makubwa" alihoji Kingunge 
Baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA kumueleza Mzee Kingunge juu ya hali ya Tundu Lissu kwa sasa ilimpa faraja mzee huyo na kusema kuwa 'Aluta Continua'


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo