Viboko 12 ukikutwa umesimama na mwanafunzi

Uongozi wa kata ya Nyehunge Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, umetolea ufafanuzi taarifa za kuwepo kwa sheria ya kuwachapa viboko 12 mtu yeyite atakayekutwa amesimama na mwanafunzi wa kike, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv diwani wa kata hiyo Charles Kalam Mbogo, amesema taarifa hizo hazina ukweli kabisa, kwani hakuna kikao cha uongozi wa kata hiyo, kilichopitisha sheria hiyo.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa kata ya Nyehunge, wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwachapa viboko 12 au faini ya shilingi 10,000 wanaume wote watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, kufuatia kukithiri kwa tatizo la wanafunzi hao kukatisha masomo kwa sababu ya kupata ujauzito.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo