Wanaume Waponea kifo baada ya kuwekewa "Limbwata" Kwenye pombe na Wanawake

WANAUME watatu waliponea kifo jijini Nairobi baada ya kutiliwa dawa za kuzubaisha, almaarufu 'mchele,’ kwenye pombe na akina dada wawili nyumbani mwao wakisherehekea Krismasi bila kutambua wawili hao walilenga kuwaibia

Watatu hao walipatikana wakiwa uchi wa mnyama na katika hali ya kutojielewa sakafuni.

Mmoja wa walinzi wa ploti wanamoishi alimkamata mwanamke mmoja katika harakati za kutoroka huku amebeba mali ya thamani, na kumrudisha kwenye nyumba hiyo kuona waliokuwemo.

Mwanamume wa nne, aliyekuwa na fahamu, alisimulia jinsi marafiki zake waliwaalika wanawake hao kwenye meza yao ya burudani katika baa moja maarufu jijini Nairobi.
Baadaye waliamua kuendeleza sherehe zao kwa nyumba ya mmoja wa rafiki yao katika mtaa wa Pipeline, Embakasi, kwa kuwa ilikuwa na 'nafasi kubwa’. Wanawake hao hawakupinga.
“Tulikuwa kwenye kilabu na tukawatongoza wasichana hao na wakakubali kwenda nyumbani nasi,” akasema.
Kulingana naye, sita hao waliabiri teksi ya Uber hadi mtaani humo usiku wa manane.
Lakini hakuweza kukumbuka chochote baada ya hapo. Hata hivyo alisema anaweza kuwatambua.
Afisa wa afya katika Hospitali ya McFinley alisema watatu hao walifikishwa kwake wakiwa hawajielewi kabisa.
Aligundua kuwa walikuwa wametiliwa kemikali kali ya kuwazubaisha kwenye pombe. Aliwaongezea sukari mwilini kujaribu kuokoa maisha yao.

na swahilihub


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo