Idara ya Elimu Sekondari yadaiwa kukumba fedha za ujenzi wa Sekondari

Idara ya Elimu Sekondari wilayani Chemba inatuhumiwa kwa ubadhiridhu wa pesa za mradi wa P4R kiasi cha 259 milion kwenye Shule ya sekondari Soya baada ya kukiuka kanuni za manunuzi ya umma
Ambapo Wananchi wa kijiji cha Soya kata ya Soya wilayani Chemba waimeilalamikia Halmashauri hiyo kutowashirikisha kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari soya kama kanuni za manunuzi ya umma ya ushirikishwaji wananchi kwenye fedha za miradi ya matokeo kama zinavyoainisha.
Akizungumza baada ya kutembelea shule hiyo kuona maendeleo ya mradi huo diwani wa kata ya Soya Mashaka Kinyogori amesema kuwa jumla ya fedha ambazo shule hiyo imepewa ni kiasi cha sh.milioni 259 kwa ajili ya ma\radi wa P4R unaotekelezwa na kanuni ya manunuzi ya umma ya ushirikishwaji wananchi.
Amesema kuwa nguvukazi kubwa ilikuwa ni kutumia fedha hizo kurudi kwa wananchi lakini mtu mmoja ndie alie amua kinyume na maelekezo yalio kwenye barua ambazo zililetwa kwenye Bodi ya shule na nakala gazeti hili inayo.
“Kanuni za manunuzi ya umma inaitaka bodi ya shule kutangaza
Msimamizi wa ukandarasi kwa kutangaza zabuni lakini kinyume chake tumeletewa Mkangarasi kutoka suma jkt kuja kuwasimamia mafundi kwa gharama kubwa kinyume na gharama halisi ambapo tungeokoa fedha hizo”alisema Mashaka
Nae Mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye kwenye ujenzi huo ni msimamizi msaidizi alipotafutwa kwa njia ya simu na hata kufika shuleni hapo hakuweza kupatikana kujibu madai hayo yaliwaowasilishwa na diwani na bodi ya shule hiyo na juhudi zinaendelea kumtafuta.
Kwa upande wake Afisa elimu sekondari ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo wa ujenzi wa shule hiyo ambaye anatuhumiwa kumleta mkandarasi huyo bila kufuata kanuni za manunuzi ya umma nae hakuweza kupatikana na juhudi zinaendelea ilikuweza kujibu tuhuma zilizoelekezwa mbele yake.
Hata hivyo wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Bilinith Mahenge kulibuka tuhuma mbali mbali zilizoelekezwa kwa Halmashauri ya chemba ambapo mkuu wa wilaya aliahidi kuzifuatilia kero hizo ambazo wananchi mbali mbali waliziibua kwenye mkutanop huo na RC.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo