Aliyekuwa mwenyeketi Wilfred Noel Kitundu na katibu wa mkoa wa chama cha ACT Wazalendo, Loth Robert Thomas mkoani Singida, wamejivua uanachama na vyeo vyao na kuhamia CCM.
Viongozi hao wamechukua uamuzi huo mbele ya mkutano mkuu wa uchaguzi CCM mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhazili mjini hapo juzi.
Kwa nyakati tofauti walisema changamoto ambazo upinzani walikuwa wakizipigia kelele, Rais John Magufuli ameendelea kuzitatua kwa ufanisi.
Viongozi hao walikabidhi kadi za vyama vyao vya zamani, kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Hadija Abood na kupewa kadi za CCM.
Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Jimson Mhagama alisema kwamba wataendelea kuwapokea wanachama wanaorejea kadi zao kutoka upinzani lakini ni lazima wafuate taratibu za chama.
