Zoezi la kupiga
chapa mifugo wilayani Makete mkoani Njombe linaendelea huku likionesha
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa
Akizungumza na blog hii Afisa Mifugo na Uvuvi wilaya ya Makete Bw. Aldo Mwapinga amesema tangu
kuanza kwa zoezi hilo hivi karibuni, bado linaendelea kwenye kata mbalimbali za
wilaya ya Makete
Amesema katika kata
ambazo bado zoezi hilo kufanyika, hamasa inaendelea kutolewa kwa wafugaji na
wananchi kuandaa vibanio kwa ajili ya kazi hiyo
Amesema pamoja na
mafanikio ya zoezi hilo kasi yake inapungua kutokana na hali ya hewa ya wilaya
ya Makete kwa sasa ambapo mvua zinaendelea kunyesha na zoezi hilo hutegemea
zaidi jua hivyo wakati mwingine linaathiriwa na hali ya hewa ya mvua
Msikilize zaidi kwenye sauti hapo chini akielezea kwa kirefu
