Imeelezwa kuwa suala
la mtuhumiwa kushikiliwa na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani kujibu
shitaka au mashitaka yanayomkabili na kuelezwa kuwa upelelezi bado
haujakamilika, ni suala la kisheria
Katika mahojiano
maalum na eddy blog mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Makete Godfrey
Gogadi amesema kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, mtu
anapotenda kosa anatakiwa kukamatwa na kupelekwa polisi ambapo atahojiwa na
polisi watakapojiridhisha na kosa hilo baada ya uchunguzi wa awali watamfikisha
mtuhumiwa mahakamani huku upelelezi zaidi ukiendelea baada ya shauri lake
kufikishwa mahakamani
Katika hatua nyingine
mwanasheria huyo ametolea ufafanuzi suala la mshtakiwa aliyetenda kosa na
kupelekwa katika mahakama ambayo haina uwezo wa kisheria wa kusikiliza shauri
hilo ambapo kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 20
kinaeleza wazi kuwa makosa yote ya kijinai ambayo yanatakiwa yasikilizwe na
mahakama kuu yahatapelekwa moja kwa moja mahakama kuu na badala yake yataanza
na usikilizwaji wa awali kwenye mahakama za kwanza
Sikiliza sauti hapo chini kwa kubofya play:-
Sikiliza sauti hapo chini kwa kubofya play:-
