Sumaye apinga Rais Kuongezewa Miaka 7

Na AGATHA CHARLES-DAR ES SALAAM 

HOJA iliyoibuliwa ndani ya Baraza la Wawakilishi, Zanzibar na kuonekana kuungwa mkono na Makamu wa Pili wa Rais visiwani humo, Balozi Seif Ali Idd, ya kutaka rais aongezewe muda wa kukaa madarakani kutoka miaka mitano hadi saba, imepingwa vikali na wanasiasa wa upinzani. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa simu jana, wanasiasa hao walisema hoja hiyo haina mashiko kwa kuwa miaka mitano iliyopo kikatiba inatosha kufanya maendeleo kwa mtu au chama kilichopo madarakani. 

Miongoni mwa wanaoipinga hoja hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na wanasiasa na viongozi wa CUF, Ismail Jussa na Nassor Ahmed Mazrui ambao wameifafanisha hoja hiyo na jambo baya, linalotoa taswira ya kuwako kwa hofu. 

SUMAYE Akizungumzia hoja hiyo, Sumaye alisema ni suala baya kwani wanaozungumzia kuongeza muda wametanguliza masilahi yao binafsi na yale ya vyama vyao. “Ni suala baya kabisa, kimsingi watu wanaozungumzia miaka saba ni wale ambao wanatafuta namna ya kutawala kwa muda mrefu kwa sababu za masilahi binafsi au ya chama. 

Miaka mitano ndiyo Katiba yetu inavyosema na ndio muda mwafaka kuwa katika miaka hiyo mnaenda kuomba kura tena kwa wananchi kama mlifanya vyema,” alisema Sumaye. 

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, alisema sababu hizo hazina uzito kwani miaka mitano inatosha kupimwa na kama ulifanya vyema utaongezewa. 

“Katiba yetu kwa sasa hairuhusu, lakini hatuwezi kusema kwa vile hairuhusu halijadiliki, lakini nasema ni kitu ambacho hakuna sababu hata ya kukisikia,” alisema Sumaye. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo